Posts

Showing posts from March, 2022

IPI DINI YA KWELI

Tukiwa mitaani waislamu na wakristo tunakula pamoja, tunacheza pamoja, tunahudhuria sherehe pamoja na tunashirikiana kwa kila hali na mali lakini ikija swala la dini hapo ndio tofauti na vita huibuka licha ya kuabundu Mungu mmoja. Tunaitana majina kama wanyama, makafiri, mapagani, mbwa... Hivi ipi dini ya kweli? Kauli ya kuwa Mungu yupo mahali popote mbona tunaibeza? Zama za mababu zetu watu walikuwa wakiomba chini ya miti, milimani na hata baharini na chakushangaza ni kuwa maombi yao yalijibiwa haraka. Siku hizi watu wanalazimishwa kuabudu makanisani na misikitini lakini bado shida zinaongezeka. Kwenye Biblia takatifu hatumuoni Baba wa imani, Ibrahim pamoja na mtumishi Ayubu wakienda kanisani lakini Mungu alikuwa akisikia maombi yao. Watu waliobarikiwa kwelikweli. Chamsingi ukifuata sheria za Mungu utaishi si hapa duniani tu bali pia ahera. Kruani tukufu inachochea upendo sawia na Bibilia takatifu sasa uhasama unatokea wapi? Hivi Mungu anakubali kweli tofauti iliyoko kati ya wakristo ...

MAISHA NI FUMBO, FUMBUA

Ili ndege waruke pamoja sharti wafanane hivyo  ukiwa na rafiki tegemea mambo mawili: kukuangusha ama kukujenga.Ili ufanikiwa katika maisha unahitajika kudondosha marafiki wapuzi na washenzi kwani wanaweza kuwa vikwazo na mizingo mizito aushini mwako. Marafiki wa kila mara nipigie, nitumie na zakutoa, nimeona kiatu kizuri si uninunulie, nahisi njaa, nataka viazi, mimi siwezi labda wewe......... ni marafiki ambao hawakuthamini na hakuna hasara ukiwadondosha. Achilia marafiki wa namna hii na uacha kauli ya tumetoka mbali kwani hawa si marafiki wa dhati bali ni wachati. Epukana na marafiki wanaopenda kusifiwa maishani. Akipanda garimoshi mazungumzo yake yote yatakuwa kuhusu garimoshi. Rafiki ambaye hupiga picha kwenye magari ya watu ili asifiwe, anayepiga picha chakula kizuri kana kwamba yeye ndo anakula, anayepiga picha kwenye mikahawa mizuri ili kututishia, nywele nzuri kumbe bandia......Watu hawa hupenda wasifiwe ilhali hali halisia analala chini ya kitanda.Rafiki kama hawa dondosha...

KENYA VIONGOZI WANAISHI LAKINI WANANCHI WANAISHA!

Hivi akili ni nini? Je madhara ya akili ni yapi? Kutenda pasipo kuelewa ni matumizi mabaya ya akili.Matumizi mazuri ya akili ni kuwa tayari kufa kwa ajili ya watu wako kinyume na viongozi washenzi na watundu ambao huhongwa chips kuku na kuweka condom zahanatini badala ya kuweka dawa ili kutibu magonjwa. Hivi condom hutibu ugonjwa gani? Hivi maisha yanasonga ama ni sisi ndio tunasonga. Inakera na kuskitikisha kuona viongozi tuliowachagua wanazembeazembea na kuhadaa wananchi, wanaongeza maafa zaidi badala ya kupunguza. Wakishikwa na homa kidogo kama mafua wanaruka na ndege kutibiwa huko London, China, Ujerumani.......huku wananchi wakisugua magonjwa sugu wengine wakipoteza maisha yao kwa kukosa kidonge cha shilingi thelathini. Hivi tunamuogopa Mungu kweli? Ni dhahiri shahiri kuwa Kenya tulibarikiwa kila kitu lakini tukalaaniwa viongizi. Ni kinaya kuwa tunateseka na baa la njaa mahali kuna ardhi yenye rotuba na maji, tunaishi bila mishahara mahali tunafanya kazi na tunalalamika ukosefu ...