KENYA VIONGOZI WANAISHI LAKINI WANANCHI WANAISHA!
Hivi akili ni nini? Je madhara ya akili ni yapi? Kutenda pasipo kuelewa ni matumizi mabaya ya akili.Matumizi mazuri ya akili ni kuwa tayari kufa kwa ajili ya watu wako kinyume na viongozi washenzi na watundu ambao huhongwa chips kuku na kuweka condom zahanatini badala ya kuweka dawa ili kutibu magonjwa. Hivi condom hutibu ugonjwa gani?
Hivi maisha yanasonga ama ni sisi ndio tunasonga. Inakera na kuskitikisha kuona viongozi tuliowachagua wanazembeazembea na kuhadaa wananchi, wanaongeza maafa zaidi badala ya kupunguza. Wakishikwa na homa kidogo kama mafua wanaruka na ndege kutibiwa huko London, China, Ujerumani.......huku wananchi wakisugua magonjwa sugu wengine wakipoteza maisha yao kwa kukosa kidonge cha shilingi thelathini. Hivi tunamuogopa Mungu kweli?
Ni dhahiri shahiri kuwa Kenya tulibarikiwa kila kitu lakini tukalaaniwa viongizi. Ni kinaya kuwa tunateseka na baa la njaa mahali kuna ardhi yenye rotuba na maji, tunaishi bila mishahara mahali tunafanya kazi na tunalalamika ukosefu wa maji mahali kuna bahari na na mito.
Mwizi hukaa jela lakini Kenya kiongozi mwizi hukaa hotelini na kula bata na mabinti wa kila aina na kubaka wagonjwa! Hivi nani asiyejua uongozi wa Idd Amin ambaye aliondoa kero la walemavu kwa kuwatupa baharini? Vijana tunahitaji kufahamu historia kwani wakati mwingine mifano mibaya ya viongozi wetu hutumika kufunza mazuri. Hivi maisha yanasonga ama sisi ndio tunasonga.
Acha nipongeze tu viongozi wachache ambao wamejitolea kimasomaso kupigania haki za wapiga kura. Najua mnakumbana na misukosuko ya kila namna lakini Mungu atawapatia nguvu.
Uchaguzi umekaribi, viongozi wamevaa ngozi ya kondoo lakini ndani ni mbwamwitu. Fikiria mara mbilimbili wakati unafanya uamuzi wako wa kura. Tunajua viongozi wetu ni matumbo kebe lakini chagua mwenye afadhali kidogo ili ucjejilaumu mbeleni.
Fanya uamuzi wa busara.
Kweli kabisa
ReplyDelete👍
DeleteKwel kabisaa
ReplyDeleteVery true
ReplyDelete💪
DeleteCondom wacha wazitumie wao viongozi wazinifu wamefumbia macho wananchi wao wakiserereka mungu yupo
ReplyDeleteAkili yapungua kila kuchao
ReplyDeleteGreat
ReplyDelete...Kwa uhakika viongozi wanafaa kuzingatia majukumu yao jinsi yapasavyo na kutimiza ahadi zao kwa wananchi kama walivyoahidi wakati wa kupiga kampeni ,hata hivyo hongera kwa kazi nzuri ila kuwa mwangalifu kwa (spelling )
ReplyDeleteWow! Kazi nzuri sana kaka.
ReplyDeleteWow
ReplyDelete