IPI DINI YA KWELI
Tukiwa mitaani waislamu na wakristo tunakula pamoja, tunacheza pamoja, tunahudhuria sherehe pamoja na tunashirikiana kwa kila hali na mali lakini ikija swala la dini hapo ndio tofauti na vita huibuka licha ya kuabundu Mungu mmoja.
Tunaitana majina kama wanyama, makafiri, mapagani, mbwa... Hivi ipi dini ya kweli? Kauli ya kuwa Mungu yupo mahali popote mbona tunaibeza?
Zama za mababu zetu watu walikuwa wakiomba chini ya miti, milimani na hata baharini na chakushangaza ni kuwa maombi yao yalijibiwa haraka. Siku hizi watu wanalazimishwa kuabudu makanisani na misikitini lakini bado shida zinaongezeka.
Kwenye Biblia takatifu hatumuoni Baba wa imani, Ibrahim pamoja na mtumishi Ayubu wakienda kanisani lakini Mungu alikuwa akisikia maombi yao. Watu waliobarikiwa kwelikweli.
Chamsingi ukifuata sheria za Mungu utaishi si hapa duniani tu bali pia ahera.
Kruani tukufu inachochea upendo sawia na Bibilia takatifu sasa uhasama unatokea wapi? Hivi Mungu anakubali kweli tofauti iliyoko kati ya wakristo na Waislamu? Mungu anatushangaza huku shetani akitucheka.
Hakuna aliyekufa akazikwa kisha akarudi duniani na kuelezea ipi dini ya kweli. Hivyo basi heshimu dini ya mwenzio
#Tsuma
Good one
ReplyDelete...Siku hizi imesalia imani ya mtu kibinafsi ,hata hivyo waumini wanafaa kuishi kwa upendo,amani na cha msingi ni kuheshimu dini la kila mmoja,hongera kwa hilo hoja👌
ReplyDeleteImani tu tosha
ReplyDelete