MAISHA NI FUMBO, FUMBUA

Ili ndege waruke pamoja sharti wafanane hivyo  ukiwa na rafiki tegemea mambo mawili: kukuangusha ama kukujenga.Ili ufanikiwa katika maisha unahitajika kudondosha marafiki wapuzi na washenzi kwani wanaweza kuwa vikwazo na mizingo mizito aushini mwako.

Marafiki wa kila mara nipigie, nitumie na zakutoa, nimeona kiatu kizuri si uninunulie, nahisi njaa, nataka viazi, mimi siwezi labda wewe......... ni marafiki ambao hawakuthamini na hakuna hasara ukiwadondosha. Achilia marafiki wa namna hii na uacha kauli ya tumetoka mbali kwani hawa si marafiki wa dhati bali ni wachati.

Epukana na marafiki wanaopenda kusifiwa maishani. Akipanda garimoshi mazungumzo yake yote yatakuwa kuhusu garimoshi. Rafiki ambaye hupiga picha kwenye magari ya watu ili asifiwe, anayepiga picha chakula kizuri kana kwamba yeye ndo anakula, anayepiga picha kwenye mikahawa mizuri ili kututishia, nywele nzuri kumbe bandia......Watu hawa hupenda wasifiwe ilhali hali halisia analala chini ya kitanda.Rafiki kama hawa dondosha haraka kwani hawatakuacha salama.

Epukana na marafiki wenye wivu kwako na wakiona mafanikio yako wananuna. Marafiki kama hawa ni hatari kuwaambia mambo ya sirini na hapa ndipo tunafeli kuongea mafanikio yetu kabla wakati wake kwa marafiki wasiofaa.

Epukana na rafiku asiyekuwa na mipango ya kuelewesha kwani mtu kama huyu kamwe hawezi angalia maisha ya usoni! Anaweza kukulaumu kwa kutoonekana baa kujivinjari. Mtu kama huyu huwa na mipango mifupi na ni hatari hata katika ndoa, anaweza vunja ndoa ndani ya lisaa, dakika hata sekunde.

Epukana na rafiki anayependa kuuza raslimali wakati hana pesa. Wengine wanauza simu na runinga ili wapate pesa za kuhongea mabnti kwenye baa. Rafiki kama huyu mtoroke haraka upesi kwani anaweza kukuuza kama Yuda alivyomuuza Yesu. Marafiki hawa ni zaidi ya sumu.

Ukichunguza maisha yako na yale ya marafiki zako hayajaachana mbali kwa sababu ukilalamika maisha ni magumu nyote mnalalamika. Huwezi kuwa na ndoto ya PHD wakati marafiki zako wanawazia kuacha darasa la tano. Ukweli mchungu ni kwamba rafiki wa dhati hawezi kukubali umshinde hivyo atafanya juu chini ili muogelea katika bahari moja.

Comments

  1. Sante kwa kuwa mkweli. Urafiki unafaa uwe wa kujenga

    ReplyDelete
  2. ...Nakubaliana na hoja zako mia kwa mia ,ni wakati ufaao wa mtu kujichunguza duara lake la marafiki ili ajuwe wepi wa kubakia nao na wa kudondosha ,rafiki wa dhati ni wakukutia moyo,kukupatia motisha na mengineo,ahsante kwa kutukumbusha kuhusu uamuzi wa rafiki tunaojihusisha nao

    ReplyDelete
  3. Marafiki wa aina hiyo hawawezi kusaidia kamwe maishani..

    ReplyDelete

Post a Comment